Nuru FM

Wanafunzi Iringa waelimishwa kuhusu afya na ukatili

17 March 2026, 9:19 am

Wanafunzi wakipatiwa elimu ya Afya na ukatili. Picha na Gerald Malekela

Changamoto ya Masuala ya afya ya uzazi na ukatili imepelekea shirika la TAHEA na Serikali kutoa elimu kwa wanafunzi.

Na Gerald Malekela

Wanafunzi wa Shule ya Ufundi Ifunda na Tanangozi Sekondari Wilayani Iringa wamepatiwa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia sambamba na kuongeza uelewa wa masuala ya afya ya uzazi na haki za vijana.

Wakizungumza na Nuru FM Baadhi ya wanafunzi walioshiriki mafunzo hayo wamesema elimu hiyo imewasaidia kufahamu namna ya kukabiliana na changamoto za ukatili wa kijinsia pamoja na sehemu sahihi za kutoa taarifa pindi wanapokumbana na vitendo hivyo.

Sauti ya Wanafunzi

Naye Makamu Mkuu wa Shule ya Ufundi Ifunda, Mwl. Leonard Magwega amesema uwepo wa vitendo vya ukatili wa kijinsia unaweza kuathiri masomo ya wanafunzi na hata kushindwa kutimiza ndoto zao.

Sauti ya Mwl. Magwega

Kwa upande wake Afisa Mradi wa REST kutoka  Shirika la TAHEA, Hidaya Juma amesema wameanzisha klabu za afya shuleni ili kuwasaidia wanafunzi kupata elimu ya afya ya uzazi na namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Sauti ya Hidaya

Naye Afisa Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Hamisi Sabuni amesema jamii inapaswa kufahamu aina kuu nne za ukatili ambazo zimekuwa zikifanya katika jamii.

Sauti ya Hamis