Nuru FM
Nuru FM
16 March 2026, 10:20 am

Moto huo ulitekekeza bidhaa za wajasiriamali ambazo bado thamani yake haijawekwa wazi.
Na Hafidh Ally
Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijafahamika umeteketeza maduka 20 ya wafanyabiashara wa bidhaa za kitalii katika eneo la Garden lililopo Manispaa ya Iringa na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara hao.
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Benjamin Sitta, amesema moto huo ulizuka ghafla majira ya saa 5 usiku wa tarehe 15 Machi 2026 huku chanzo chake kikiwa bado hakijafahamika.
Mh. Sitta amesema Ofisi yake kwa kushirikiana na mamlaka husika inaendelea kufanya tathmini ya haraka ili kubaini ukubwa wa athari na hasara iliyosababishwa na ajali hiyo ya moto.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara ambao maduka yao yametekea na moto wameeleza kusikitishwa na tukio hilo lililotekekeza maduka 20.

Aidha Jeshi la zimamoto na uokoaji lilifika katika eneo la tukio mara baada ya kupata taarifa ya moto huo na kuanza juhudi za kuuzima Kwa kushirikiana na baadhi ya wananchi waliokuwepo karibu na eneo hilo.
Eneo hilo ambalo ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa linakadiriwa kuwa na wafanyabiashara wa bidhaa za utalii wasiopungua 50, ambapo baadhi yao wamepoteza mali zao kufuatia tukio hilo.