Nuru FM

Wanawake Mufindi waonywa kuacha kuwapiga wanaume

7 March 2026, 10:29 am

Mwenyekiti wa Uwt Wilaya ya Mufindi mwenye Skafu shingoni akiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. Picha na Fredrick Siwale

“Wanaume Wilaya ya Mufindi wamekuwa wakikutana na vipigo na wanakaa kimya”

Na Fredrick Siwale

Wanawake Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wametakiwa kuacha tabia ya kuwapiga waume zao ili kukuza ustawi katika Jamii.

Hayo yamezungumzwa wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo yamefanyika Kata ya Mninga na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mufindi Bi. Marcelina Mkini na kuongeza Kuwa wakati wanaadhimisha siku ya wanawake duniani ni vyema wanawake wakawa na mipaka ya kuwaheshimu waume zao na kuacha mara moja tabia ya kuwapiga.

Sauti ya Mwenyekiti

” Ipo tabia ya wanawake kuwapiga waume zao pale wanapoonywa, hii haifai, na mara nyingi wanaume ni wakimya hata wakipigwa Huwa hawasemi” Alisema Mkini.

Aidha Amewataka Wanawake hao kujikita katika shughuli za kiuchumi kwa kuendesha miradi bila kusahau jukumu mama la kusimamia elimu kwa Watoto wao.

Sauti ya Mwenyekiti UWT

Kwa upande wake Mh. Asunta Mtende Diwani wa Vitimaalum Mninga alimshukuru Mgeni rasmi kwa kukubali kufika na kujumuika pamoja na Wanawake wa kata hiyo ambayo imekuwa mwanzo wa kukuza ustawi katika Jamii.

Sauti ya Asunta

Katika maadhimisho hayo wanawake waliamua kutoa Zawadi ya mbuzi Kwa Diwani Mstaafu wa Kata ya Mninga Mh. Festo Mgina ambaye ni Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa kuwatumikia vema.