Nuru FM

Bei ya bidhaa yapaa Kwaresma na Ramadhan

6 March 2026, 8:50 am

Baadhi ya wafanyabiashara wakiendelea na shughuli zao katika soko kuu Iringa.

Na Elika Matonya na Telesia Chalamila

Wafanyabiashara wa soko kuu Mkoani Iringa wameeleza hali halisi ya biashara na aina ya bidhaa zinazouzika katika msimu huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan pamoja na kwaresma.

Wakizungumza na Nuru FM Baadhi ya Wafanyabiashara hao wameeleza bidhaa zinazouzika msimu huu wa mfungo ni pamoja na mihogo, magimbi na viazi, licha ya kukabiliana na ongezeko la bei za bidhaa hizo kutoka kwa Wakulima.

Sauti ya Wafanyabiashara

Aidha Wafanyabiashara hao wametoa ushauri kwa wakulima kupunguza bei za bidhaa kwani kunafanya baadhi ya wafanyabiashara kushindwa kukidhi manunuzi ya bidhaa hizo.

Sauti ya Wafanyabiashara Iringa

Nao baadhi ya wanunuzi wa bidhaa katika soko kuu Manispa ya Iringa wameeleza changamoto kubwa wanazozipitia katika msimu huu wa mfungo ni kupanda bei kwa baadhi ya bidhaa.

Sauti ya Wanunuzi Iringa

Ikumbukwe kuwa mwezi huu ni mwezi wa mfungo kwa wakristo na waislamu hivyo wakulima na wafanyabiashara  wachukulie kama kipindi cha kawaida kama hapo awali ili kujipatia Baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu.