Nuru FM

Wananchi 7000 Iringa kupata bima za afya

13 February 2026, 10:12 am

Zoezi la ugawaji wa Bima za afya likiendelea. Picha na Joyce Buganda

Mpango huu umekuja ili kuhakikisha wananchi wapata huduma za afya bila vikwazo.

Na Joyce Buganda

Wananchi 7827 kutoka  Halmashauri ya Wilaya ya Iringa yenye   kata 28 wamashatambuliwa na wanatarajiwa kunufaika na mpango wa bima kwa wote kampeni ambayo inaendelea nchi nzima yenye lengo la kuhakikisha wananchi  wanapata huduma za matibabu pasipo vikwazo vya kifedha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhakiki, usajili na ugawaji  wa bima za afya kwa wote wasio na uwezo  lililofanyika katika  kijiji na kata ya kisin’ga Wilayani Iringa Mratibu wa bima ya afya kutoka Halmashauri ya Iringa Dkt Renatha Kato amesema halmashauri ya wilaya hiyo inaanza zoezi hilo kwa awamu ya kwanza ambayo wameanza na  watu wasiojiweza makundi maalumu kama watu wenye ulemavu,  Wazee, wajawazito na watoto ambayo kwa awamu hii watagharamiwa na serikali.

Sauti ya Kato

Awali Afisa Tarafa Kutoka Tarafa ya Ismani Benitho Kayugwa  ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Iringa amesema  serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania imeona wananchi wake wanavyopata tabu hasa katika sekta ya kiafya na wameanza na makundi maalumu ambao watapata kadi za bima ya afya ambayo watapata matibabu bure, huku akiendelea kuwasisitiza wananchi hao kuzitunza kadi hizo,

Sauti ya Kayugwa

Nao baadhi ya wanufaika wa Mpango wa Bima ya afya kwa wote wameishukuru serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuwapatia kadi hizo huku wakisema mwanzoni walikuwa wakishindwa kwenda kutibiwa kutokana na ghalama kubwa za matibabu.

Sauti ya Wanufaika

Ikumbukwe kuwa mpango wa bima ya afya kwa wote ni mpango wa Taifa ambao unalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu bila kuathiriwa na ghalama kubwa   ambapo kwa wale wanaolilipia watatakiwa  kulipia shilingi 150,000 ambayo itajumuisha watu 6 katika kaya.