Nuru FM
Nuru FM
28 January 2026, 5:30 pm

Na Joyce Buganda
Serikali mkoani Iringa imeanzisha Mfuko wa Uhifadhi wa Milima ya Tao la Mashariki EAMCEF unaolenga kufadhili wakulima na wafugaji katika jitihada za uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Hayo yamezungumzwa na Afisa mazingira mkoani Iringa Golyama Bahati na kuongeza kuwa kuna vigezo vinavotumika ni wakulima na wafugaji kutengeneza vikundi ili kuwafikia kwa urahisi.
Kwa upande wao Wanufaika wa mradi wa EAMCEF wanasema wamefaidika, ikiwemo kupata bayo-gesi inayosaidia katika kilimo na ufugaji.
Naye Afisa Mifugo Mkoa wa Iringa Bw. Chacha Mwita anatoa wito kwa wafugaji kuacha kufuga kwa mazoea badala yake wapende kuijfunza vitu vipya.
Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kubwa kwa Wakulima na wafugaji hivyo wanahitaji mikakati thabiti, shirikishi, na uwajibikaji wenye tija.
