Nuru FM
Nuru FM
15 January 2026, 12:22 pm

Kundi la watoto wenye ulemavu linapaswa kupata elimu kama watoto wengine.
Na Joyce Buganda
Wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu mkoani Iringa wameshauriwa kuwapeleka watoto wao waliofikiwa umri wa kwenda shule Ili kupata haki ya msingi na kufikia ndoto zao.
Ushauri huo umetolewa umetolewa na Mkurugenzi wa kituo kinachotoa huduma za utengamao mkoani Iringa cha Lebao’s Kids Foundation Theophil Muyinga wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema kuwa wazazi wasikate tamaa kuona wamepata watoto au mtoto mwenye ulemavu hivyo wawape haki za msingi kama elimu.
Aidha Muyinga amewasihi wazazi wasikate tamaa kuona wana watoto wenye ulemavu kwani wanauwezo wa kufanya shughuli mbalimbali pia kuwasaidia kuwainua kwa pamoja.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa chama cha watu wenye Ualbino nchini Alfred kapole amewataka wazazi kuhakikisha watoto wenye ulemavu wa ualbino wanawapeleka watoto wao kupata elimu kwani usalama upo kila sehemu.
Hayo yamekuja kutokana na baadhi ya wazazi kuwaficha watoto wenye ulemavu na kutowapa haki zao za kimsimgi ikiwemo elimu.