Nuru FM
Nuru FM
13 January 2026, 10:38 am

“Mazingira ya uwekezaji yakiwa mazuri lazima wawekezaji waongeze uzalishaji wa bidhaa”
Na Hafidh Ally
Serikali ya imepongezwa kwa kufanya mageuzi makubwa na kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji jambo linalochochea ukuaji wa shughuli za uzalishaji, kuongeza ajira na kupanua wigo wa mapato ya Serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Manispaa ya Iringa, Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Food and Beverage na Ivori Ltd, Suheil Esmail Thakore, amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeboresha kwa kiasi kikubwa mazingira ya kufanya uwekezaji nchini na kuondoa vikwazo visivyo vya lazima.
Amesema pamoja na maboresho hayo, Serikali imeimarisha mahusiano ya kimataifa, hatua ambayo imewasaidia wawekezaji kuuza bidhaa zao nje ya nchi kwa urahisi zaidi, kuongeza ushindani katika masoko ya kimataifa na kukuza pato la makampuni pamoja na uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Kuhusu ajira, Thakore amesema kiwanda chake kimeongeza ajira kwa vijana kutokana na maboresho ya mazingira ya uwekezaji na upanuzi wa soko ambapo kiwanda hicho kinatarajia kuongeza uzalishaji wa bidhaa kwa asilimia 100 ifikapo mwisho wa mwaka 2026.

Amebainisha kuywa hatua itakachangia zaidi ajira kwa jamii inayozunguka kiwanda hicho, kukuza mapato ya Serikali na ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla.
Aidha, amewataka Watanzania kujenga na kuimarisha utamaduni wa kupenda na kutumia bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi, akisema hatua hiyo itasaidia kukuza viwanda vya ndani.
Amesema kuwa Kiwanda chao kinafanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi jambo lililopelekea kupata vyeti mbalimbali vya kutambua kazi wanazofanya.
