Nuru FM

Wadau kukarabati miundombinu ya shule ya Lusinga

28 December 2025, 8:09 pm

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Mwenyekiti wa Kundi la Wanalusinga wanaoishi nje ya kijiji, Greyson Nyamoga, wakikabidhi msaada. Picha na Adelphina Kutika

“Ubora wa miundombinu ya madarasa utasaidia wanafunzi wajifunze katika mazingira bora”

Na Adelphina Kutika

Uchakavu wa majengo ya Shule ya Msingi Lusinga Katika Halmashauri ya wilaya ya kilolo mkoani Iringa umeendelea kuwa changamoto kubwa kwa mazingira ya ujifunzaji na ufaulu wa wanafunzi, hali iliyoibua haja ya kuchukua hatua za haraka kupitia ushirikiano wa jamii na wadau wa maendeleo.

Akizungumza katika tamasha hilo, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Mwenyekiti wa Kundi la Wanalusinga wanaoishi nje ya kijiji, Greyson Nyamoga, amesema majengo ya shule yamechakaa kwa kiwango kinachoathiri moja kwa moja mazingira ya kujifunzia na ufaulu wa wanafunzi.

Sauti ya Nyamoga

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Lusinga, Jakobo Mbwelwa, ametoa wito kwa wananchi wote wa kijiji hicho waliopo nje ya Lusinga kujiunga na kundi la Wanalusinga wanaoishi nje ili kushirikiana kuleta maendeleo ya pamoja.

Sauti ya Mwenyekiti

Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Lusinga, Amasha Kisoma, amesema Shule ya Msingi Lusinga ni miongoni mwa shule za zamani katika eneo hilo na majengo yake yamechakaa kwa kiasi kikubwa.

Sauti ya Mtendaji

Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa shule,Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Lusinga, Athuman Hassan, amesema majengo yaliyopo hayaridhishi kwa mazingira ya elimu, hivyo kushirikiana kwa wazazi na jamii ni jambo lisiloepukika.

Sauti ya Mwalimu

Kwa upande wao, baadhi ya wazazi walioudhuria tamasha hilo wamesema wako tayari kushiriki katika michango na shughuli za ujenzi kwa kuwa elimu ya watoto wao ipo hatarini endapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

Sauti ya Wazazi

Hata hivyo Katika tamasha la mwaka huu, kundi hilo limeungana na wananchi kwa kula chakula cha pamoja na kutoa kompyuta pamoja na mashine ya kuchapisha (printer) kwa Shule ya Msingi Lusinga ili kuboresha huduma za kielimu, pamoja na kutoa mahitaji kwa watoto na wazee wenye mazingira magumu.