Nuru FM

RC Kheri asisitiza bima ya afya kwa wote

17 December 2025, 2:37 pm

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James akizungumza na watumishi wa afya. Picha na Hafidh Ally

Bima ya afya imetajwa kuwa msaada kwa wananchi kupata huduma bora za afya.

Na Hafidh Ally

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya zote mkoani hapa kuhakikisha kuwa vituo vyote vya afya vinafungwa na kuanza kutumia mifumo ya kidijitali, ili kufanikisha utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.

Akizungumza katika kikao cha kuwajengea uwezo watumishi juu ya utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote mkoani Iringa, Kheri James amesema matumizi ya mifumo hiyo yataongeza uwazi, ufanisi na ufuatiliaji sahihi wa huduma za afya, sambamba na kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa haraka na kwa usawa bila usumbufu.

Sauti ya RC kheri

Kheri James amesema matumizi ya mifumo hiyo ni muhimu katika kuondoa changamoto za ucheleweshaji wa huduma, upotevu wa mapato pamoja na malalamiko ya wananchi wanaotumia huduma za bima ya afya.

Sauti ya RC kheri

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt Sylivia Mamkwe amesema kuwa ni vyema watumishi wa afya wakahakikisha wamatoa huduma bora za afya kwa wananchi hasa kusimamia mfumo wa bima ya afya kwa wote.

Sauti ya RC Mganga

Bima ya Afya kwa Wote ni mpango wa Serikali ya Tanzania unaolenga kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za afya bora na kwa gharama nafuu, bila kujali kipato chake au eneo analoishi.