Nuru FM

Wazazi waaswa kuwalinda watoto wakati wa likizo

5 December 2025, 10:58 am

“Ulinzi kwa watoto wakati wa likizo ni vyema ukazingatiwa ili kuwalidhi shidi ya matukio ya ukatili”

Na Fredrick Siwale

Wazazi na Walezi Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa wametakiwa kuwalinda Watoto wao kipindi cha likizo ya mwisho wa mwaka 2025 baada ya Shule kufungwa ili kuwakinga na matukio ya ukatili. 

Hayo yamezungumzwa katika  mkutano wa Wazazi wa Wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Mafinga na Afisa wa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Mafinga Nuru Kwayi, na kuongeza kuwa Wazazi wanatakiwa kuweka Ulinzi na Usalama kwa Watoto wao kipindi chote cha mapumziko. 

Sauti ya Afisa maendeleo

Amewataka Wazazi kuacha tabia ya kuwaruhusu Watoto kuangalia televisheni au kuachiwa simu zao za mkononi ili kuwaepusha na matumizi mabaya ya mtandaoni. 

“Lakini Wazazi ugomvi wenu na Lugha zisizo za staha msizionyeshe kwa mbele ya Watoto mnawafundisha tabia za hovyo” Alisema Kwayi. 

Aidha amewataka wazazi kuanza kufanya maandalizi ya kuwanunulia watoto wao mahitaji mazuri ya shule ili na wao wawe katika saikolojia nzuri sambamba kuzingatia lishe bora dhidi yaio.

Sauti ya Afisa maendeleo

Kwa Upande wake Afisa wa Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mufindi Bi. Mary Kailo, amewataka Wazazi kuhakikisha Watoto wao wanapata nafasi ya kucheza na siyo kuwafungia ndani kwani hupelekea kuwehuka pale wanapopata nafasi ya kucheza na wenzao.

Sauti ya Afisa Dawati

Awali Mwenyekiti wa Wazazi wa Shule ya Msingi  Mafinga Bi. Sifa Gerana amesema tabia ya baadhi ya Wazazi kutopeleka chakula Shuleni ili hali wao wanaishi na kula vizuri na kushiriki shughuli za Sherehe za Harusi na zinginezo ni ukiukwaji wa haki za Watoto.

Sauti ya Mwenyekiti