Nuru FM
Nuru FM
26 November 2025, 10:46 am

Matukio ya ukatili yamekuwa yakidumaza ustawi wa watoto na wanawake.
Na Joyce Buganda
Wadau na Wajumbe wa mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA sehemu ya 2 wametakiwa kutumia uzoefu wao katika kuelimisha jamii kupinga na kutokomeza vitendo vya ukatili kwa kundi hilo katika jamii.
Akizungumza katika kikao cha kamati ya MTAKUWWA sehemu ya 2 kilichofanyika katika ukumbi wa siasa ni kilimo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Robert Masunya amesema anaamimi wadau na wajumbe kwa ngazi ya halmashauri watakwenda kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kutokomeza ukatili.
Awali Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi Gladnss Amulike amesema muongozo wa MTAKUWWA II umezingatia ujumuishi wa ushiriki wa wanaume katika kupinga ukatili kuanzia ngazi ya kaya.
Kwa upande wake Loveness Mayingu ambaye ni Mkaguzi wa Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la jinsia na watoto amesema wao kama dawati wanaendelea kutoa elimu kwenye jamii ili kupumguza vitendo vya ukatili.
Ikumbukwe kuwa kikao hicho ni muendelezo wa Mkoa wa Iringa katika hatua na ngazi za Halmashauri zote kutengeneza mpango mkakati wa 2024/25- 2028-29 ya kupambana na na vitendo fvya ukatili dhidi ya wanawake na watotokuanzia ngazi kata vijiji na mitaa.