Nuru FM
Nuru FM
23 September 2025, 8:30 pm

Bweni hilo litasaidia wanafunzi kupata Muda wa kusoma na kuongeza ufaulu.
na Joyce Buganda
Walimu wilaya ya Iringa wametakiwa kuhakikisha wanawasimamia ipasavyo wanafunzi kulinda na kutunza miundombinu ya shule.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mabweni katika Shule ya Sekondari William Lukuvi iliyopo Kijiji Cha Magozi kata ya Ilolo mpya Sitta amesema serikali itaendelea kujenga na kuboresha miundombinu ili wanafunzi wasome katika Mazingira mazuri hivyo ni wajibu kwa walimu kuhakikisha wanawahimiza wanafunzi kuwa watunzaji wa rasilimali hizo kwa maendeleo ya sasa na baadae.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi huo Mkuu wa Shule ya Sekondari William Lukuvi Mwl Godwin Isaya amesema mwaka wa masoko 2026 wanatarajia kuanza kidato Cha 5 kwa tahasusi za CBG na HKL huku serikali ikiipatia shule hiyo zaidi ya shilingi milioni 380 kupitia mradi wa Sequip ili kujenga mabweni mawili, matundu 10 ya vyoo na Madarasa manne

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw. Robert Masunya ameutaka uongozi wa shule kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya kuhifadhia maji Ili kuwa na akiba pindi yanapokatika ili kukabiliana na changamoto iliyopo sasa.