Nuru FM

George akutwa amejinyonga Iringa

11 September 2025, 9:53 am

Picha na EATV

Changamoto ya watu kujiua inapaswa kufanyiwa uchunguzi na kutatuliwa ili kupunguza vifo katika jamii.

Na Godgrey Mengele

Mwanaume mmoja ajulikanaye kwa jina la George Severin Manga mkazi wa Kitongoji cha Kihesa katika Kijiji cha Ilambilole amekutwa amejinyonga kwa kile kinachodhaniwa ni migogoro ndani ya ndoa yake.

Akizungumza na Nuru Fm kwenye kipindi cha Nyambizi Mwenyekiti wa kitongoji cha Kihesa Kijiji cha Ilambilole, Ndugu Hosiana Mhanze amesema kuwa sababu za mwanaume huyo kujinyonga hazijabaanika haraka licha ya kuwa na masuluhisho kadhaa ya ndoa yake katika ofisi za kijiji hicho.

GODFREY MENGELE ANA TAARIFA ZAIDI……………

MWISHO