Nuru FM
Nuru FM
2 September 2025, 12:47 pm

Na Godfrey Mengele
Taasisi binafsi Mkoa Iringa zimepatakiwa kuisaidia jamii kujikwamua kiuchumi kwa kuwafikishia huduma mbalimbali.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James wakati wa hafla ya kukabidhi bajaji 32 zenye thamani ya shilingi milion 315 zilizotolewa kwa mkopo na benki ya CRDB Tawi la Mkwawa kwa kushirikiana na Ofisi ya Umoja wa Bajaji wilaya ya Iringa UMABAI.
Kheri James amesema kuwa sekta binafsi zinapaswa kuisaidia jamii kwa kuunga mkono serikali ili kundi la vijana liendelee kufanya kazi na kujipatia kipato cha mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.

Aidha Kheri James amebainisha kuwa serikali itaendela kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi kwa vijana kwa kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi pamoja na sekta binafsi kulifikia kila kundi.
Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James amewataka madereva wa bajaji kujiepusha na matukio ya uhalifu kupitia vyombo hivyo na kuripoti pale yanapotokea ili jamii ibaki salama.
Melabu Kihwele ni mwenyekiti wa Umoja wa Bajaji Wilaya ya wake amesema kuwa wamejipanga kutokomeza mikataba kandamizi waliyokuwa wanaingia madereva bajaji na wamiliki wa usafiri huo.
