Nuru FM

Wazazi Iringa waaswa kuwapa elimu watoto

31 August 2025, 9:17 am

 
Wazazi na walezi mkoani Iringa wametakiwa kuhakikisha wanawapa elimu bora watoto wao kwani ndio urithi wa kudumu ili taifa liwe na wasomi wenye hekima na busara.

Akizungumza katika mahafali ya nne katika shule ya  awali na msingi Luindo Mkurugenzi wa  shule hiyo  Lusungu Ndondole amesema yeye na timu yake wamejipanga kutoa elimu bora  huku akiomba ushirikiano baina yao na wazazi na walezi uendelee.

Sauti ya Mkurugenzi

Naye Mtaaluma Mkuu wa shule ya  awali na Msingi Luindo  Mwalimu Nasir Sadick amewaasa wanafunzi Kuendelea kujifunza pia kutumia maarifa yao kama taa ya maisha yao ya kielimu.

Sauti ya Sadick

Wakisoma risala wahitimu wa darasa la saba kwa mwaka huu wamehitimu jumla ya wanafunzi 78 wasichana 43 na wavulana 35 huku wakijivunia mwaka pia wameainisha baadhi ya changamoto zilizopo shuleni hapo ni pamoja na ukosefu wa viwanja vya michezo na ukosefu wa tanuli la kuchomea taka ngumu.

Sauti ya Msoma Risala

Akizungumza kwa niaba ya wazazi mmoja wa wazazi ameushukuru uongozi wa shule hiyo kwa kuwapa malezi na upendo waliowaonyesha watoto wao kwa Miaka 7.

Sauti ya Mzazi

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Biashara mkoa wa Iringa Bw Ibrahim Makwata amewapongeza wahitimu hao kwa kuhitimu na kuendelea kuwahimiza wazazi kuwekeza elimu kwa watoto wao pia amesema changamoto zote ame..sikia na watazifanyia kazi

Sauti ya Meneja