Nuru FM

MTAKUWWA kuwashirikisha wanaume kutokomeza ukatili Iringa

14 August 2025, 10:20 am

Wadau wa kutokomeza ukatili wa kijinsia Mkoani Iringa. Picha na Joyce Buganda

Mpango wa kutokomeza ukatili wa kijinsia unalenga kuongeza usawa wa kijinsia katika jamii.

Na Joyce Buganda

Serikali imekuja na Mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili wakijinsia kwa wanawake na watoto MTAKUWWA awamu ya pili mpango unatekelezwa nchi nzima kwa kumtaka mwanaume aingie katika kutokomeza ukatili nchini.

Akizungumza katika mafunzo yaliowajumuisha maafisa ustawi wa jamii maendeleo ya jamii, polisi jamii wadau wa watoto na watumishi wa afya kutoka Halmashauri  ya Wilaya ya Mufindi na Mafinga Mji Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Iringa Martin Chuwa amesema wameamua kuwashirikisha wanaume kwenye mpango huu ili kupunguza kasi ya ukatili.

Sauti ya Chuwa

Grace Simalenga  ni Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa amewashukuru shirika la SOS  childrens Villages kwa kuandaa mafunzo hayo ma kuongeza  na kusema kuwa   wameaanza kukutana na makundi haya kwa sababu ndio makundi ambayo yapo kwenye jamii moja kwa moja  hivyo wanaamini elimu itafika kwa uharaka Zaidi.

Sauti Grace

Kwa upande wake Afisa Miradi wa Shirika la SOS Childrens Villages   mkoa wa Iringa Vikta Mwaipungu amesema wao kama SOS  wapo kwenye jamii katika kuinua na kusaidia makundi mbalimbali kama watoto, mabinti waliojifungua katika umri mdogo na kuwainua kiuchumi wanawake.

Ikumbukwe kuwa MTAKUWWA  ni mpango wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ambapo kwa mwaka huu ni hii ni awamu ya pili awamu ya kwanza iliisha mwaka jana 2024.