Nuru FM

Wafanyabiashara wapewa elimu ya utambuzi biashara

4 August 2025, 6:44 pm

Wajasiriamali wakipewa elimu ya biashara. Picha na Joyce Buganda

Kujiasajili na kupata kitambulisho cha kufanyia biashara husaidia kutambulika na kufanya biashara kwa uhuru.

Na Joyce Buganda

Wafanyabiashara ndogondogo Mkoa wa Iringa wamepata elimu kuhusiana na utambuzi na usajili wa biashara  ili wawe na uelewa kuhusu shughuli wanazozifanya.

Akizungumza na Maafisa usafirishaji kutoka Kituo cha Bajaji cha Mashine tatu, Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Iringa Bi. Rehema Mchunga amesema kigezo kikubwa cha kuwa mfanyabiashara na kuwa na kitambulisho cha Mjasiriamali.

Sauti ya Afisa Usafirishaji

Aidha Afisa Mikopo kutoka Benki ya NMB amesema Serikali imechagua benki ya NMB kwa ajili ya kutoa mikopo nafuu yenye riba ndogo hivyo mfanyabiashara inabidi awe umetimiza vigezo vyote ikiwemo kitambulisho cha mjasilimali.

Sauti ya Afisa Mikopo

Kwa upandewake Afisa Elimu  na Mawasiliano kwa Mlipakodi mkoa wa Iringa Shaga Gagunda amesema wao kama Mamlaka ya mapato Tanzania  TRA  wanawatembelea  watu wote wanaofanya biashara halali kuendelea kushiriki katika kuchangia kulipa kodi pamoja na kurasimisha biashara zao.

Sauti ya Afisa Elimu