Nuru FM
Nuru FM
2 August 2025, 7:25 am

Sekta ya kilimo imetajwa kuwa sekta muhimu jambo linalopelekea vijana kutakiwa kuwekeza huko.
Na Godfrey Mengele
Vijana Mkoani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wamehimizwa kuwekeza nguvu katika kilimo ili kujikwamua kiumchumi na kufikia malengo yao.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Saumu Kweka katika Warsha iliyowakutanisha vijana iliyoandaliwa na Mradi wa YEFFA (Youth Empowerment for Food and Farming Advancement) unaotekelezwa na shirika la RUCODIA kwa ufadhili wa AGRA (Alliance for a Green Revolution in Africa), ikiwa na lengo la kuwaelimisha kuhusu fursa ya mikopo ya halmashauri, upatikanaji wa pembejeo bora na masoko ya mazao yao.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya vijana Mkoa wa Iringa Atilio Mganwa amesema kuwa Sera ya maendeleo ya Vijana na Sera ya Serikali kwa ujumla imeweka mazingira mazuri kwa wadau mbalimbali wanaosaidia vijana ili kusaidia kundi hilo kufikia malengo yao.
Meneja Mradi wa YEFFA (Youth Empowerment for Food and Farming Advancement) Jackson Jasson, amewataka vijana Mkoani Iringa kukitazama kilimo kama biashara halali na yenye uwezo wa kubadili maisha yao endapo watajiandaa kifikra na kitaalamu.
Mradi wa YEFFA unatekelezwa na shirika la RUCODIA kwa ufadhili wa AGRA (Alliance for a Green Revolution in Africa), ukiwa na lengo la kuwafikia vijana zaidi ya 54,000 katika mikoa ya Iringa, Njombe na Songea.