Nuru FM
Nuru FM
31 July 2025, 12:39 pm

Fursa ya utoaji Mikopo kwa vijana imetakiwa kutekelezwa bila ubaguzi Ili kuwanufaisha wahusika.
Na Godfrey Mengele
Watumishi wa halmashauri za Mkoa wa Iringa wametakiwa kuacha urasimu pindi wanapowahudumia vijana hasa wanapochangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10 ili kutotengeneza mazingira ya rushwa.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Estomin Kyando ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo alipowakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James katika maonyesho ya ujuzi, fani na ajira kwa vijana kwa ajili ya kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupitia mradi wa Skills for Employment Tanzania (SET) unaotekelezwa na taasisi ya Swisscontact, ikiwa ni sehemu ya kusaidia nguvu kazi ya taifa kwa kuwapatia maarifa, ujuzi na fursa za kazi.

Masunga Sumbi ni Afisa habari kutoka Shirika la Swisscontact amesema kuwa tamasha hilo limekuwa na mafanikio makubwa ambapo takribani vijana elfu 2 wamefikiwa na lengo lilikuwa kuwafikia vijana elf 3 katika shughuli mbalimbali zilizofanyika.
Kwa upande wao baadhi ya vijana wanufaika wa maonyesho ya ujuzi, fani na ajira wameishukuru taasisi ya Swisscontact kupitia mradi wa Skills for Employment Tanzania kwani maonyesho hayo yamewasaidia katika kutangaza bidhaa wanazo tengeneza.
