Nuru FM

World Vision yakabidhi Cherehani 24 Wasa

30 July 2025, 9:04 am

Wanufaika wa Cherehani zilizotoka Shirika la World Vision Tanzania wakizijaribu. Picha na Adelphina Kutika

Msaada wa Cherehani kwa Vijana hao ni katika juhudi za kuunga Mkono Vijana na wanawake kukuza uchumi wao.

Na Adelphina Kutika

Jumla ya cherehani 24 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 zimekabidhiwa kwa vikundi vitatu vya vijana katika kata ya Wasa, Halmashauri ya wilaya ya Iringa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha kiuchumi na kupunguza utegemezi wa kifamilia unaochangia vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Akizungumza Katika hafla yakukabidhi vifaa hivyo,Meneja wa Kanda ya Kati na Kusini wa Shirika la World Vision Tanzania Pudensiana Rwezaula    amesema  kuwa uwezeshaji wa vijana  ni njia mojawapo ya kudumu ya kupambana na umaskini na ukatili wa kijinsia katika jamii.

Sauti ya Meneja

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Saumu Kweka amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau kama World Vision ili kuhakikisha vikundi hivyo vinapata mikopo ya asilimia kumi kutoka halmashauri, ili kuviwezesha kuongeza mitaji na kupanua shughuli zao za kiuchumi.

Sauti ya Afisa Maendeleo

Hata hivyo Cherehani zilizotolewa na shirika la World Vision kwa vijana wa kike 34 waliokuwa wakipatiwa mafunzo ya ufundi wa ushonaji katika chuo cha ufundi kilichopo katika Parokia ya Wasa ambapo wanufaika hao wamesema msaada huo utasaidia  kuboresha maisha yao, kujitegemea kiuchumi na na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya familia na jamii

Sauti ya Wanufaika