Nuru FM
Nuru FM
27 June 2025, 3:37 pm

Kozi Mpya ziilizozinduliwa na Chuo Cha Muce zinalenga kutatua changamoto ya ajira kwa vijana.
Na Godfrey Mengele
Chuo kishiriki cha Elimu Mkwawa Iringa { MUCE } Kimezindua kozi mpya za kitaaluma 7 {Post Graduate Degree Programmes} kwa ajili ya msimu mpya wa masomo 2025-2026 ikielezwa kuwa lengo ni kuwafikia wahitaji wengi ili kutatua changamoto ya ajira iliyopo.
Akizungumza na waandishi wa habari Deusdedit Rwehumbiza Profesa Mshiriki na Naibu Ras wa Chuo kishiriki cha Elimu Mkwawa Iringa amesema uanzishwaji wa kozi hizo umezingatia maoni ya wananchi, wadau wa elimu na wahitimu waliotoka chuoni ambapo iliwasaidia katika kufanya maboresho ya kozi hili ili kutatua matatizo ya kijamii.
Profesa Rwehumbiza amesema kuwa kozi zilizotangazwa za { Post Graduate Degree Programmes} ni saba na mbili umahiri {Masters Degree Programme} na kozi zilizosalia ni uzamili {PHD Programmes}.
Deusdedit Rwehumbiza Profesa Mshiriki na Naibu RAS wa Chuo kishiriki cha Elimu Mkwawa Iringa amewakaribisha waombaji kuchangamkia kuomba nafasi za kusoma kozi hizo kwani gharama ni nafuu akitanabaisha kuwa chuo kina mazingira mazuri ya kufundishia miundombinu bora, na walimu weledi.
Kwa upande wake Dk Chacha Steven Chacha Mkurugenzi wa Shahada za uzamili kutoka Chuo kishiriki cha Elimu Mkwawa Iringa amewaondolea shaka baadhi ya watu wanaodhani chuo hicho kinafundisha kozi ya ualimu pekee na kwamba wana kozi tofauti tofauti.