Nuru FM
Nuru FM
24 June 2025, 1:14 pm

Kutokana na changamoto wanazopitia wajane, serikali imeamua kufanya utafiti ili kuzitafutia ufumbuzi.
Na Adelphina Kutika
Serikali imezindua mwongozo mpya wa uratibu wa wajane wenye lengo la kulikomboa kundi hilo dhidi ya changamoto za ukatili wa kijinsia na vikwazo vya kiuchumi.
Mwongozo huo umetangazwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Iringa yenye kaulimbiu Isemayo “Tuimarishe Fursa za Kiuchumi Kuchochea Maendeleo ya Jamii.”

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kilolo Bi Rebecca Sanga Nsemwa aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa amesema maadhimisho hayo yamejumuisha wajane kutoka halmashauri zote tatu yakiambatana na utoaji elimu ya fedha na haki ya wajane
Nae mmoja wa wajane mkoani Iringa ameishauri jamii kuhakikisha waandika wosia ili kuondoa migogoro kwa familia pindi wazazi wanapofariki.

Hata hivyo mwongozo huo unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii, kiuchumi na kisheria kwa wajane.