Nuru FM

Wastaafu Iringa waomba kupewa mikopo

24 June 2025, 12:46 pm

Afisa Uhusiano wa Azania Benki tawi la Iringa Abdulkarim Chande akizungumza na wastaafu Iringa. Picha na Godfrey Mengele.

Zoezi la utolewaji wa Mikopo kwa wazee limetajwa kuwasaidia katika kukuza uchumi wao.

Na Godfrey Mengele

Katika kuhakikisha wastaafu nchini wanaendeleza maisha yao kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi wamezitaka benki nchini kuwakopesha kiasi kikubwa cha fedha kwani mahitaji sasa yamepanda thamani.

Wito huo umetolewa na Mwl Stanslaus Mhongole katika kikao kilichoandaliwa na Benki ya Azania kilichofanyika katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Iringa ambapo ameitaka benki hiyo kufikiria namna ya kuwapatia mikopo mikubwa ya fedha huku akipendekeza kima cha juu kianzie Tsh Milion 10 kwani uwezo wa kulipa wanao kutokana na serikali kuwalipa penseni nzuri.

Sauti ya Mwenyekiti

Mhongole amesema kuwa baadhi ya taasisi za kifedha zimekuwa na hofu juu ya maisha wanayoishi wastaafu mara baada ya kustaafu kazi na kuwaondolea shaka kuwa sasa wanaishi maisha marefu na wanaweza kulipa mikopo hiyo.

Sauti ya Mhongole

Akijibu hoja zilizotolewa na wastaafu hao Afisa Uhusiano wa Azania Benki tawi la Iringa Abdulkarim Chande amesema benki hiyo imekuwa rafiki kwa kundi hilo kwani inatambua ukomo wa maisha ya mwanadamu apangayo ni Mwenyezi Mungu pekee.