Nuru FM
Nuru FM
19 June 2025, 1:33 pm

Mipango ya elimu kwa Mtoto wa kike imeanza Kutekelezwa Nchini Ili kukuza ustawi.
Na Joyce Buganda
Maafisa elimu nchini wametakiwa kutekeleza miradi ya Campagn For Female Educatiom CAMFED ili kufanikisha malengo ya mtoto wa kike kupata elimu bora kwa ustawi wa maisha na jamii kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya siku 2 yaliofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Manispaa ya Iringa mgeni rasmi mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa limu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Suzan Nussu amesema maafisa hao wakasimamie vyema ipasavyo ardhi walizonazo kwa ajili ya miradi iliaonzishwa na shirika la CAMFED.
Aidha Mkurugenzi wa Miradi na ushirikiano kutoka shirika lisilokuwa la kiserikali Campaign For Female education CAMFED Anna Sawaki amesema mradi upo katika mikoa 10 na halmashauri 35 wamekutana kujadili juu ya utekelzaji wa miradi ya elimu ambayo inafanywa na CAMFED.
Kwa upande wao baadhi ya maafisa elimu wamesema wanaendelea kushirikiana na CAMFED ili kuemdeelea kuborha na kutimiza ndoto ya mtoto wa kike nchini.