Nuru FM

Afariki Dunia akishiriki tendo la ndoa

12 June 2025, 9:38 am

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Banga aliyethibitisha kifo cha Kabupa.

Na Mwandishi wetu

Mwanaume mmoja Mkazi wa Kijiji cha Igelehedza kilichopo kata ya Ilembula Wilayani Wanging’ombe Mkoani Njombe Erasto Raphaely Kabupa mwenye umri wa miaka 50 amedaiwa kufariki dunia wakati akishiriki tendo la ndoa na mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuwa mke wa mtu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo na kueleza kuwa lilitokea siku ya tarehe 8 juni 2025 majira saa mbili usiku,ambapo marehemu alikuwa na mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa katika nyuma ya kulala wageni ambapo wakati wakiendelea na tendo alizidiwa gafla na kukimbizwa kituo cha afya Ilembula na kukutwa ameshapoteza maisha.

Sauti ya Kamanda Banga

Kamanda Banga amesema kutokana na aina ya tukio hilo Jeshi la Polisi haliwezi kumkamata mwanamke aliye kuwa pamoja na marehemu huyo,huku akitoa wito kwa wanandoa kuwa waaminifu na kuheshimu ndoa zao.

Sauti ya Kamanda Banga

Diwani wa kata ya Ilembula Hezron Myale amesema kupitia taarifa ya familia ambayo imetolewa wakati wa mazishi ambayo yamefanyika leo imebainisha kuwa sababu ya kifo cha Eresto Kabupa ambaye pia ameacha mjane na watoto ni tatizo la moyo ambalo limekuwa likimsumbua kwa mda mrefu huku akiwataka wanandoa kuwa waaminifu kwenye ndoa zao ili kulinda uchumi na familia zao.

Sauti ya Diwani Myale

Nao baadhi ya wananchi mjini Makambako Pascal Shauri na Justini Mwanganya wamesema changamoto kubwa kwa sasa kwa wanandoa ni kukosa kuaminiana,maelewano na uvumilivu hali ambayo inapelekea kusalitiana na kuleta adha katika familia na jamii kwani visa vya mapenzi ndio sababu ya mauaji.

Sauti ya Wananchi

Erasto Kabupa ambaye alikuwa ni mwenye ulemavu wa miguu uliosababishwa na ajari enzi za uhai wake alikuwa akijishughulisha na shughuli za ufundi wa ushonaji viatu na baadaye usafirishaji abiria kwa kutumia bajaji kutoka ilembula kwenda halali.