Nuru FM

Huduma za kitabibu kuwanufaisha Wanamufindi

5 June 2025, 6:14 pm

Baadhi ya wananchi Wilaya ya Mufindi wakiwa tayari kupatiwa matibabu. Picha na Ayoub Sanga

Madaktari Bingwa wa Samia wametajwa kuwa msaada kwa wananchi Wilaya ya Mufindi waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata matibabu.

Na Ayoub Sanga

Watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi iliyopo Mkoani Iringa wamesema Ujio wa madaktari Bingwa wa Dkt Samia ni neema kwao na kwa wananchi wanaowahudumia katika sekta ya afya.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi John Nchimbi amesema Ujio wa madaktari bingwa utasaidia pia kupata mafunzo kwa madaktari walioko katika vitio vya kazi na kurahisisha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.

Sauti ya Nchimbi Mganga Mfawidhi

Naye Dkt. Fredy Michael ambaye ni dakatri wa kinywa na Meno katika Hospitali hiyo amesema uwepo wa kambi hiyo unawasaidia wananchi kunufaika na huduma za kisasa za matibabu.

Sauti ya Dkt. Michael

Dkt Fredy amebainisha kuwa wamepata ujuzi wa kisasa wa namna ya kuziba meno badala ya kung’oa kwa muda mfupi na mrefu ili kupunguza magonjwa ya fizi.

Sauti ya Dkt. Michael

Kwa upande wao baadhi ya Wananchi waliofika katika Hospitali ya Wilaya ya Mufindi wameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kupelekewa Madaktari bingwa ambapo program hii imewapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu kufata huduma za kibingwa katika hospitali kubwa.

Sauti ya Wananchi Mufindi