Nuru FM
Nuru FM
26 May 2025, 12:34 pm

Wananchi wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma za afya wataanza kuneemeka na huduma za afya.
Na Ayoub Sanga
Zaidi ya shilingi milioni 400 zimetumika katika ujenzi wa Kituo cha afya cha Mninga kilichopo kata ya Mninga, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Akiwasilisha taarifa mbele ya wajumbe wa Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Afisa Mtendaji kata ya Mninga Bi Addah Lwangili amesema jumla ya fedha zilizopokelewa kwajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Mninga ni shilingi million 498.
Akiwa ameongozana na kamati ya siasa Mkoa wa Iringa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba, ametoa wito kwa wakandarasi wanaojenga jengo la kisasa la mama na mtoto kuhakikisha linakamilika kabla ya mwezi wa 9 ili kuwarahisishia akina mama kupata huduma kwa wakati.
Akizungumza na wananchi waliokusanyika katika kituo hicho, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Daud Yassin amesema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuboresha huduma za msingi, ikiwamo afya, ili kuwafikia wananchi wote kwa urahisi na ufanisi.
Aidha Kituo hicho kinatarajiwa kuhudumia zaidi ya wananchi 15,000 waliokuwa wakikumbana na changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya, ikiwemo kutembea zaidi ya kilomita 15 kufuata matibabu kama ambavyo hapa wananchi wakieleza
Hata hivyo Kituo cha afya cha Mninga kinajumuisha majengo ya wagonjwa wa nje (OPD), maabara, wodi ya wazazi, chumba cha upasuaji, na wodi za kulaza wagonjwa, hivyo kutarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya mama na mtoto na kuongeza ustawi wa jamii kwa ujumla.