Nuru FM

Vijana 120 kunufaika na mradi wa usindikaji bidhaa za chakula Iringa

18 May 2025, 7:46 pm

Moja ya Viwanda vya usindikaji wa bidhaa za chakula.

Na Adelphina Kutika

ZAIDI ya vijana 120 kutoka kata 18 za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wanatarajia kunufaika na mradi wa uendelezaji wa ujuzi wa kujiajiri kupitia usindikaji wa bidhaa za chakula.

Hayo yameelezwa katika hafla ya ufunguzi wa mradi huo ambao unaratibiwa na Shirika la Build Sustainable Bussiness Idea kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) ambapo Edwin Muta Mratibu wa mradi huo amesema umelenga kuwawezesha vijana ujuzi utakaowasaidia kuimarisha shughuli zao.

Sauti ya Mratibu

Akimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Iringa, Afisa Vijana Manispaa ya Iringa, Atilio Mganwa amesema Serikali ipo tayari wakati wote kushirikiana na wadau wa maendeleo kwa maslahi mapana ya vijana na jamii kwa ujumla.

Sautu ya Afisa Vijana

Naye Meneja wa SIDO Mkoa wa Iringa, Johari Masengi amesema SIDO wakati wote imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Serikali na Taasisi nyingine katika jamii na kuwainua vijana.

Sauti ya Meneja

Mradi wa uendelezaji wa ujuzi wa kujiajiri kupitia usindikaji wa bidhaa za chakula unatekelezwa kwa kipindi cha miezi 9 lengo ni kuwajengea uwezo vijana kushiriki kwenye shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kilimo cha biashara.