Nuru FM
Nuru FM
6 May 2025, 9:09 pm

Na Adelphina Kutika
Jeshi la polisi mkoni Iringa linamshikilia Joseph Yustino Mhilila mkazi wa mtaa wa Lukosi Kata ya Mtwivila kwa tuhuma za kumuua mtoto wake timotheo Mhulikwa (6) aliyepotea tangu tarehe 1 mwezi wa nne 2025.
Akizungumza na Nuru FM Mwenyekiti wa mtaa wa lukosi Kenedi Mahona anasema ni wiki tatu zimepita tangu mzazi huyo alipotoa taarifa kuwa mtoto wake hapatikani lakini baada ya upelelezi wa jeshi la polisi amekiri kuhusika kwenye mauaji ya mwanae.

Kwa upande wake mmliki wa nyumba alipokuwa akiishi mkazi huyo maximilian luhwago anasema kuwa kijana huyo alikuwa anajishughulisha na kazi ya usafirishaji bodaboda huku akieleza namna alivyo mpokea mtoto huyo kutoka kwa mzazi mwenzie na kile kilichotokea.
Nae Afisa usafirishaji Laurent Lukosi ambaye alikuwa wakifanya kazi ya usafirishaji Manispaa ya Iringa amesema kuwa kwa kushirikiana na jeshi la zima moto Mkoa wamefanikiwa kutindua shimo la choo na kukuta vipande vya mwili wa mtoto huyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa SACP Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo ameeleza kuwa kijana huyo alimkata vipande vipande mtoto wake na kumtupa katika shimo la choo.
