Nuru FM

TCCIA Kilolo yaja na maonyesho Ya kilimo Na biashara mwezi Mei

18 April 2025, 5:10 pm

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo BiRebecca Sanga Nsemwa akizungumza kuhusu maonesho ya TCCIA. Picha na Joyce Buganda.

Na Joyce Buganda

Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo TCCIA imeandaa maonesho ya Biashara, viwanda na kilimo yatakayofanyika Wilayani Kilolo Mkoani Iringa kuanzia Mei 21 hadi Mei 25, 2025 yakilenga kuwapatia nafasi wahusika wa sekta hizo kuonesha shughuli wanazozifanya ili kupanua wigo wa uzalishaji na masoko.

Akifungua kikao cha Majadiliano ya maonesho hayo Katika Ukumbi wa chuo cha Maendeleo FDC Kilichopo Ilula Wilayani Kilolo, Mkuu wa Wilaya hiyo Rebecca Sanga Nsemwa amewaalika Wananchi wa hiyo na Mkoa wa Iringa na maeneo jirani kushiriki katika maonesho hayo kwani yatakuwa na tija kwa makundi mbalimbali yatakayoshiriki.

Sauti ya DC

” maonesho haya yatatupatia fursa sisi wanakilolo kuonyesha vitu na bidhaa zetu tunazozifanya au kuonyesha mazao tunayoyazalisha Wilayani kwetu hivyo hima tuamke tushiriki,” Amesema DC Sanga.

‎Aidha Katibu wa chemba ya biashara Kilimo na viwanda TCCIA Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Painetho Madembwe ambao ndiyo waandaji wa Maonyesho hayo, amesema maonesho hayo yatatoa fursa kwa wananchi wa Kilolo kujifunza na kupata tija zaidi katika biashara zao.

‎”Naamini kama kila kundi litashiriki maonesho haya kikamilifu basi kila mmoja wetu atajifunza kutoka kwa mwenzake na hivyo ndiyo biashara zinavyoendeshwa,” amesema Madembwe

Naye Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo TCCIA Wilaya ya Kilolo, Charles Chavala, ameeleza kuwa wamejipanga kufanikisha kwa ufanisi maonesho hayo, huku wakiamini kuwa Wakazi wa Wilaya ya Kilolo watanufaika na maonesho hayo katika makundi tofauti, ikiwa ni pamoja na Wakulima, Wafugaji na Wafanyabiashara.

Sauti ya Mwenyekiti

Kwa upande wao baadhi ya Wafanyabiashara katika eneo la Ilula Mtua ambapo yatafanyika maonesho hayo wameonesha kufurahishwa na mpango huo wakiamini kuwa watapata fursa za kupata faida.

Sauti ya Wafanyabiashara

Maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya chuo cha Maendeleo FDC kilichopo eneo la Ilula Mtua lililopo Wilayani Kilolo yakiwa na kaulimbiu ya “Kilolo mpya, Fursa mpya za uwekezaji na kilimo cha kibiashara kuchochea maendeleo”.