Nuru FM

Vijana Iringa wahimizwa kusoma vitabu ili kuongeza maarifa

17 April 2025, 11:18 am

Muonekano wa Maktaba ya kisasa Mkoani Iringa. Picha na Alex Sona

Na Zaitun Mustapha na Catherine Soko

Vijana  mkoani  Iringa wameshauriwa kuwa na mwamko wa kusoma vitabu mbalimbali ili  kuweza kukua kiakili, kongeza ufahamu na maarifa.

Hayo yamezungumzwa na baadhi ya vijana Manispaa ya Iringa ambapo wameelezea ni kwa namna gani  usomaji wa vitabu umekua na manufaa  katika maisha ya kila siku.

Muonekano wa ndani wa maktaba ya Mkoa wa Iringa

Aidha wamesema vijana wengi wanashindwa kwenda Maktaba kuchukua vitabu ili wasome na kupata maarifa na badala yake wanatumia mda mwingi kuperuzi mitandaoni.

Kwa upande wake Kaimu mkutubi wa maktaba ya mkoa Iringa Bi. Elizabeth Rionjo amekiri kuwa vijana wengi hawatumii maktaba kujisomea vitabu ambapo kwa sasa serikali imetoa mwongozo wa mtu mzima kulipia shilingi elfu 10 na wanafunzi shilingi elfu 5 kwa mwaka mzima.

Sauti ya Mkutubi

MWISHO