Nuru FM
Nuru FM
16 April 2025, 11:04 am

Na Geaz Mkata na Rogasia Kipangula
Wafanyabiashara wa Mchele Manispaa ya Iringa wamesema kuwa Bei ya Mchele imepanda kuanzia shilingi 2000 mpaka shilingi 3200 kwa kilo moja.
Wakizungumza na Nuru FM baadhi ya wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wamesema kuwa bei hiyo imepanda kutokana na upatikanaji wake kuwa shida kwa sasa hasa baada ya mfungo wa ramadhani Kutamatika.
Aidha wamesema kuwa Toka mvua zimeanza kusumbua mchele umepanda bei jambo linalopelekea wateja kulalamikia bei kuwa kubwa.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wa chakula Manispaa ya Iringa maarufu MamaLishe wamesema kuwa baada ya mchele kupanda bei wateja wao bado wanataka kuuziwa Wali kwa shilingi 1500.
