Nuru FM
Nuru FM
16 April 2025, 9:51 am

Na Joyce Buganda
Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wametakiwa kujifunza lugha ya kichina kwani kupitia lugha hiyo wanaweza kupata fursa mbalimbali ikiwemo ufadhiri katika masomo yao.
Akizungumza katika mashindano ya taranta za kichina ya wanafunzi wa vyuo vikuu duniani yaliofanyika katika taasisi ya Confucius chuo Kikuu kishiriki cha elimu cha Mkwawa RAS wa chuo kikuu Kishiriki cha elimu mkwawa Prof. Method Samwel Semiono amesema kwa chuo cha mkwawa pekee wanafunzi 70 wamejisajili kujifunza lugha hiyo.

Aidha RAS Semiono amesema taaisi hiyo ilianza rasni mwaka 2013 huku akiwaasa wanafunzi kutumia fursa ya kujifunza lugha hiyo kwani kuna fursa nyimgi ikiwmo ufadhili wa masomo pindi ukionyeha nia ya kujifunza lugha hiyo.
Hata hivyo Dr. Musa Hans ni mwenyekiti kutoka Confucius ya chuo kikuu cha Dar es salaam amesema ni vizuri kujifunza lugha hii kwani lengo kuu ni kujenga madaraja baina ya wanafunzi na makampuni mbalimbali ya kichina ili kukuza ajira nchini.
Ikumbukwe kilele cha mashindano haya kitafanyika tarehe 20 mwezi mei katika chuo kikuu cha Dar es salaam na washindi wawili watapata zawadi mbalmbali ikiwa pamoja na kwenda kutembelea nchi ya china.
