Nuru FM
Nuru FM
11 April 2025, 3:20 pm

Na Joyce Buganda
Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM Taifa komredi Mohamed Kawaida ameanza ziara ya siku mbili mkoani Iringa lengo likiwa ni kukagua Miradi ya chama pamoja na Kukiimarisha Chama kiwe kwenye umoja na mshikamano hasa katika kipindi Cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2025.
Akizungumza wakati wa Kuzindua Maduka 11 ya biashara yaliopo vibanda vya CCM Iringa mjini Komredi kawaida ameipongeza jumuiya ya umoja wa vijana kwa mradi huo kwani kutaongeza mapato katika jumuiya huku amewaasa vijana hao Kuendelea kushikamana pamoja na kudumisha amani katika maeneo yao kwani vijana ndiyo nguvu ya Taifa.

Awali katibu wa Umoja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa Aisha Mpuya amesema mradi huo wa Maduka ni mradi wa umoja wa vijana na wamewapa kipaumbele vijana na wananchi pia ambapo Kuna flemu ilighalimu milioni 6 ambapo milango hii itagharimu shilingi Milioni 2 na nusu kwa mwezi kwa mlango na milioni 4 na nusu hii kwa mwezi itagharimu laki 1 na nusu ambapo elfu 50 wanalipa kwa jumuiya kwa mlango.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa vijana UVCCM mkoa wa Iringa Agrey Tonga amewashukuru vijana kwa ushirikiano wanaonyesha katika mradi huo japo mwanzoni kulikuwa na changamoto huku akiwaasa kugombea nafasi mbali mbali ifikapo uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.
Komredi Kawaida ameanza ziara ya siku mbili mkoani Iringa na atatembelea Miradi mbalimbali pamoja na kuzungumza na vijana hii yote ni Kuendelea kukijenga chama Cha Mapinduzi hasa katika kipindi hiki Cha kuelekea uchaguzi Mkuu ifikapo mwezi oktoba mwaka huu.
