Nuru FM
Nuru FM
8 April 2025, 8:22 am

Na Editha Maximillan na Israel Nchimbi
Wafanyabiashara wa zao la Viazi Mviringo katika Soko Kuu Manispaa ya Iringa wamesema kuwa bei ya zao hilo imepanda ikilinganishwa na ilivyokuwa katika mwezi wa Ramadhan.
Wakizungumza na Nuru Fm baadhi ya Wafanyabiashara wa zao hilo katika Soko kuu wamesema kuwa kwa sasa mzunguko wa biashara siyo mzuri ikilinganishwa na kipindi cha mfungo wa ramadhani huku bei ya viazi ikipanda kutoka shilingi elfu 3500 kwa kisado mpaka shilingi elfu 5.

Aidha Bei ya gunia la viazi kwa sasa inadikia shilingi elfu 65 kwa gunia jambo lililopelekea pia wauzaji kupandisha bei.
Emanuel Galala Ni miongoni mwa wanunuzi wa Viazi Mviringo katika soko kuu amesema kuwa viazi viliuzika zaidi katika kipindi cha mwezi wa Ramadhan na kwa sasa upatikanaji wake siyo kama ilivyokuwa wakati huo.