Nuru FM

Mafinga Mji yatoa elimu ya afya na lishe kwa jamii

26 March 2025, 10:53 am

Uongozi wa Halmshauri Mafinga Mji wakitoa elimu ya Afya na lishe kwa wananchi wao. Picha na Fredrick Siwale

Na Fredrick Siwale

Katika kuadhimisha siku ya Afya na Lishe, Halmashauri ya Mji Mafinga imetoa elimu ya namna ya kupambana na changamoto za lishe kwa wakazi wa Mtaa wa Mkombwe uliopo Kata ta Boma.

Akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya siku ya Afya na lishe kwa vitendo katika mtaa wa Mkombwe kata ya Boma Halmashauri ya Mji Mafinga Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Afisa lishe wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Bw.Salumu Atlas amesema elimu hiyo itasaidia wazazi kuwa na uelewa wa kuandaa lishe bora dhidi ya watoto.

Sauti ya Afisa

Kwa Upande wake Bi.Laiza Mbogo Afisa maendeleo ya Jamii kata ya Boma amekiri kuwepo kwa udumavu na kuitaka Jamii kushiriki siku za maadhimisho na kuacha tabia ya kuuza vyakula.

Sauti ya Maendeleo

Awali Afisa lishe kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bw. Ashery amefafanua kuwa baada ya mtoto kukutwa na udumavu, Mzazi atapewa utaratibu wa kumuandalia chakula kwa kufuata mlo kamili.

Sauti ya Afisa

Aidha Bw.George Mtandi Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mkombwe,aliwashukuru Wazazi kwa kujitokeza na kupeleka Watoto ,Wajawazito na Wazee katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika mtaa huo.