

19 March 2025, 12:36 pm
Na Adelphina Kutika
Mkoa wa Iringa umeanzisha kampeni ya kutoa elimu kwa umma ili kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Mpox, ambao umekuwa tishio kwa afya za wananchi.
Akizungumza katika hafla ya kutoa elimu hiyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Silvia Mamkwe, ameeleza kuwa Mpox ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Mankey Pox na unaambukizwa kwa njia ya kugusana na mtu aliyeambukizwa.
Kwa upande wake Abubari Chalamila amesema kama viongozi wa dini watahakikisha wanawaelimisha waumini kupitia nyumba za ibada ili kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi
Msaidizi wa Askofu kupitia Kanisa la KKKT Dayosisi ya Iringa Askali Mgehekwa amesema kuwa kama waumini watashirikiana na vyombo vya habari kuelimisha kuacha kusalimiana kwa kupeana mikono ili kusaidia jamii kuwa salama.
MWISHO