Nuru FM

Wajasiriamali wanawake waagizwa kutumia fursa za kiuchumi

17 March 2025, 11:30 am

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba akizungumza na wanawake wajasiriamali. Picha na Adelphina Kutika

Na Adelphina Kutika

Wajasiliamali Wanawake Mkoani Iringa wamehimizwa kutumia fursa zilizopo kuwekeza katika maeneo yao ili kuongeza upatikanaji wa masoko na huduma za kibiashara ili kukuza uchumi na kuzalisha vyanzo vingi vya ajira hapa nchini.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba wakati akifungua  mafunzo kwa Wajasiliamali Wanawake yaliyoandaliwa na TWCC kwa ufadhili wa TradeMark Africa katika Ukumbi wa Royal Hotel Uliopo Manispaa ya Iringa na kusema kuwa serikali inaendelea kuwajengea mazingira bora ya biashara ili kugeza fedha za kigeni na ajira.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa

Awali akiwasilisha taarifa mbele ya mgeni rasmi rais wa CHEMBA ya wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Bi. Mercy Silla amesema lengo la mafunzo hayo  ni kuwaelezea wajasiliamali wanawake  na vijana  kutambua  taratibu za kufanya biashara  kwenye soko huru la Africa (AFCFTA) .

Sauti ya Rais

Pendo Ndumbaro  ni Mwenyekiti wa CHEMBA ya wanawake Wafanyabiashara Mkoa wa Iringa (TWCC) amesema mafunzo hayo yanakwenda kuwa msaada kwa wajasiliamali wanaozalisha bishaa zenye ubora ili zikashindanishwe kwenye soko huru la Africa kutokana na kuondondolewa  kwa vikwanzo .

Sauti ya Pendo

Kwa upande  wao baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mafunzo hayo akiwemo Theresia Masao ambaye ni mfugaji nyuki ameiomba serikali kuondoa kodi kwa wajasiliamali wadogo wanaonza kwani zimekuwa kikwazo kuinuka kichumi

Sauti ya Mjasiriamali

MWISHO