

6 March 2025, 12:47 pm
Na Adelphina Kutika
Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Avetisyan, ameonesha dhamira ya kuleta uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania, hasa katika sekta ya kilimo, ili kuongeza fursa za ajira na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Balozi Avetisyan amesema hayo akiwa ziarani mkoani Iringa, ambapo amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Peter Serukamba na kufanya mkutano pande hizo mbili na kujadili fursa za kuimarisha uhusiano kati ya Urusi na Mkoa wa Iringa, hususan katika sekta za utalii, kilimo, usafiri na elimu.
Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira bora kwa wawekezaji, jambo ambalo litachochea mataifa mengine kuja kuwekeza kwa wingi.
Aidha, Meneja Mkuu wa Browns Tea Plantation, Nashon Kamnyungu, alieleza kuwa ujio wa Balozi Avetisyan ni fursa muhimu kwa upatikanaji wa soko la chai kimataifa na kuongeza thamani ya zao la chai.
MWISHO