

28 February 2025, 8:46 am
Na Joyce Buganda
Kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu makatibu, siasa, uenezi na mafunzo w CCM ngazi ya kata na matawi wilayani kilolo ukanda wa juu wamepewa semina elekezi ili kuwaandaa na kuwakumbusha kutekeleza majukumu yao Kulingana na katiba na Kanuni za Chama hicho na kuelewa mipaka yao ya kazi.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya kilolo, Katibu siasa, Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Iringa Joseph Lyata amesema makatibu uenezi wana wajibu wa kuhakikisha heshima ya chama inatunzwa vyema.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kilolo Justin Nyamoga amewatoa rai kwa wenezi kuhakikisha miradi iliopo kwenye maeneo yao ya utawala inalindwa na kusimamiwa ipasavyo pamoja na kukisema vyema Chama Cha Mapinduzi.
Hata hivyo katibu siasa na uenezi wilaya ya kilolo Reminius Sanga amesema ukanda wa juu wa kilolo una makatibu wenezi wa matawi na kata 83 amaamini semina hiyo imewaingia na anaamini wanakwenda kuwafikishia wananchi wa maeneo yao ujumbe.
Semina hiyo imekuwa chachu kwa Waenezi hao kuwa Mstali wa mbele kukisemea Chama, kuitaja na kuielezea Miradi Mikubwa ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya CCM ili Wananchi wawe na uelewa wa namna Fedha zinavyotumika Kutatua kero, vilio na Changamoto zinazowakabili.
MWISHO