Nuru FM

Mwanilwa akabidhi bati 40 ujenzi wa nyumba ya watoto yatima Zizini

9 February 2025, 1:27 pm

Mariam Mwanilwa Mwenye kilemba cha njano akikabidhi bati 40 kwa dada wa familia ya watoto yatima. Picha na Shaffih Mhina

Na Mwandishi wetu

Mjumbe wa Mkutano Mkuu UWT Taifa Wilaya ya Handeni Bi Mariam Mwanilwa amechangia Bati 40 kwa familia ya watoto Yatima 6 iliyopo Mtaa wa Zizini Kata ya Chanika Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Mabati Hayo, Bi Mariam Mwanilwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Marafiki wapenda Maendeleo Wilaya ya Handeni MMAHA, amesema kuwa baada ya Balozi wa Maji Mkoa wa Tanga Habib Mbota maarufu Moja kwa Moja kumshirikisha kuhusu Nyumba ya watoto hao kuezuliwa na upepo mkali baada ya kubwa kubwa kunyesha aliamua kuunga Mkoani juhudi ambazo alizianzisha za kuwapatia makazi mapya.

” Mimi nilipigiwa simu na Moja kwa Moja kuhusu kuwapatia makazi watoto hawa sita Yatima na kweli nikaona nije hapa na wanawake wenzangu wa UWT kupaona na kukabidhi Mabati haya Ili nyumba iezekwe na watoto wahamie” Alisema Mwanilwa

Kwa upande wake Habibu Mbota ambaye ni Madau wa Maendeleo Mkoa wa Tanga alisema kuwa alivyoona watoto hao hawana nyumba aliamua Kuanza ujenzi kwa gharama zake mpaka kufikia hatua ya lenta kwa asilimia 50 ndipo wadau Wengine wakamuunga Mkono akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Awali Mwenyekiti wa CCM Kata ya Chanika Said Mwingwa amewapongeza Mariamu Mwanilwa na Habibu Mbota kwa kujitoa kuwasaidia watoto hao ambao wanapotia wakati mgumu baada ya nyumba Yao kuezuliwa na Upepo.

Naye Rahma Daudi ambaye ni Dada wa Familia hiyo Mwenye umri wa miaka 18 alimshukuru Bi Mariam Mwanilwa na Habibu Mbota kwa kuwasaidia kupata nyumba hiyo ambayo ikikamilika itawafanya waishi katika Mazingira salama.