

4 February 2025, 9:33 am
Na Hafidh Ally
Halmashauri ya Mji Mafinga Mkoani Iringa imeomba kupatiwa Bilioni 11.7 kwa ajili ya matengenezo ya barabara korofi katika jamii.
Hayo yamezungumzwa na Meneja wa Wakala wa barabara vijijini (TARURA) Wilaya ya Mufindi Mhandisi Richard Sanga wakatia akitoa ripoti ya utekelezaji wa bajeti ya TARURA katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitisha bajeti ya mwaka 2025/2026 na kuongeza kuwa fedha hizo zitaweza kutatua kero ya ubovu wa moundombinu ya barabara Mafinga Mji.
Akichangia hoja hiyo Diwani Kata Ya Saohill, Mheshimiwa Denis Kutemile ameiomba Tarura kuboresha miundombinu ya barabara ili huduma za kijamii ziweze kufikiwa.
Naye Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Mji Mafinga , Mheshimiwa Regnant Kivinge ameitaka Tarura kuhakikisha bajeti iliyopendekezwa inatatua changamoto zote za barabara kwani wana imani na utendaji kazi ambao wameuonesha katika mji huo.
MWISHO