Nuru FM

Tuna Finance Hub kutoka UoI kuwanufaisha vijana

20 January 2025, 12:13 pm

Umoja wa Tuna finance Hub wakiwa katika picha ya Pamoja na vijana. Picha na Joyce Buganda

Na Joyce Buganda

Umoja wa Tuna Finance Hub kutoka Chuo Kikuu cha Iringa wamejidhatiti kuhakikisha vijana wa Iringa wanakombolewa kiakili na kifikra katika utafutaji na jinsi ya kupata maendeleo katika sekta mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo  katika chuo kikuu Cha Iringa mmoja wa waanzilishi wa Tuna finance hub Helman Minazi amesema lengo lao ni kutoa elimu ya fedha hasa kwa wanafunzi na kawafanya vijana kuwa wepesi katika kuziona fursa za kimaendeleo.

Sauti ya Mwanzilishi

Aidha Mhadhiri kutoka chuo kikuu Cha Iringa Bi Teresia Josephat amesema wao kama chuo wanashirikiana vyema na Tuna finance hub kwa sababu katika masomo  yaliyotolewa  chuoni hapo ni pamoja na jinsi ya kutunza fedha katika mifuko mbalimbali ya uwekezaji, wajibu wa kifedha na uchumi katika jamii.

Sauti ya Mhadhiri

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wamesema wanaishukuru  Tuna finance hub kwa kuwapa elimu ya fedha kwani wengi wao walikuwa wanapata fedha na kutumia vibaya.

Sauti ya Washiriki

Hafla hiyo imehudhuriwa na Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo mkoani Iringa.