Nuru FM

One Acre Fund yatoa Miti Kilolo kutunza mazingira

17 January 2025, 12:46 pm

Kiongozi wa One Acre Fund akizungumza kuhusu utoaji wa Miti. Picha na Joyce Buganda

Na Joyce Buganda

Wananchi wa kijiji cha Itimbo, kata ya Ihimbo wilayani Kilolo Mkoani Iringa wamenufaika na msaada wa miti uliotolewa na Shirika la One Acre Fund.

Wakizungumza wakazi wa kijiji hicho wakati wa kupokea miti hiyo Wamesema miti hiyo itawasaidia kuongeza kipato na kuchangia jitihada za kutunza mazingira katika eneo lao.

Sauti ya Wananchi

Kwa upande wake Afisa Habari wa Shirika la One Acre Tanzania LTD, Dorcas Tinga amesema shirika hilo limepanga kusambaza miti milioni nne mwaka huu katika mikoa ya Iringa, Mbeya, Njombe, na Songwe na kuwawezesha wakulima kuboresha mashamba Yao.

Sauti ya Afisa habari

Kwa upande wake Afisa Misitu kutoka kitengo cha Maliasili wilaya ya Kilolo, Bw. Aige Mwilafi, amesema, “Kila mwaka wanalenga kupanda miti zaidi ya milioni 12 kwa kushirikiana na Shirika la One Acre Fund.”

Sauti ya Msimamizi

Naye Msimamizi wa Miradi ya miti ya malipo na hewa ya ukaa kutoka Wilaya ya Kilolo, Wakatae Nyamba amesema, wanatoa miti kwa wananchi kwa lengo la kurutubisha ardhi na kuwasaidia kupata kipato kutokana na mazao ya miti kama matunda.

MWISHO