Nuru FM

Iringa wakusanyika kuenzi utamaduni wa Wahehe

31 December 2024, 10:01 am

Wakazi wa Kijiji cha Lisinga wakiwa katika picha ya Pamoja baada ya kupeana taratibu za Mila na desturi za kabila la wahehe. Picha na Adelphina Kutika

Na Adelphina Kutika

Wakazi wa Kijiji cha Lusinga, Kata ya Dabaga, Wilaya ya Kilolo, wanaoishi katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wamekusanyika kwenye kijiji hicho kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa lengo la kukumbushana malezi bora na maadili yenye misingi ya mila na desturi za Wahehe.

Akizungumza kwenye hafla ya Lusinga mhadhili wa Chuo Kikuu Cha Kilimo (SUA) Morogoro Greyson Nyamoga ambaye pia ni mwenyekiti wa kundi hilo la Wanalusinga amesema kuwa kusanyiko hilo limefanyika kwa lengo la kuelimishana kuhusu jinsi jamii inavyoweza kuendelea kuenzi na kutunza urithi wa Wahehe ili kizazi kijacho kifuate nyayo za mababu zao.

SAUTI YA NYAMOGA

Mzee Daudi Kimata , ambaye ni miongoni mwa viongozi wa kijiji hicho, amesisitiza kuwa, “Mila na desturi za Wahehe zilikuwa zikifundisha  kuhusu umoja, kujali, na kuheshimu wazee tofauti na ilivyosasa kwa vijana.

SAUTI Y BABU DAUDI

Kwa upande wake bibi Sesilia Luhwago amewapongeza wana kundi la lusinga kuchukua hatua ya kuwakutanisha wananchi wa kijiji hicho kwani inasaidia kuwaelimisha vijana juu ya malezi bora ya kimaadili ili kulinda utamaduni na ustawi wa jamii.

SAUTI YA BIBI SESILIA

Mwalimu Richard ni Mmoja wa wana kundi la Lusinga ametoa shukrani  kwa wazee wa kijiji hicho kwa kutoa ushirikiano katika kuhakikisha sherehe hiyo kufanyika.

SAUTI YA RICHARD

Hata hivyo  sherehe hiyo, vijana wamepata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wazee kuhusu historia ya jamii yao, pamoja na maadili muhimu kama vile upendo, heshima, na mshikamano huku wakitafakari na kujivunia utamaduni wao wa kimaadili.

MWISHO