Nuru FM

Wanaume Iringa walalamikia kupigwa na wake, kuwekewa limbwata

10 December 2024, 12:31 pm

Miongoni wa mwa wanaume mkoani Iringa wakilalamikia kitendo cha wake zao kuwawekea limbwata kwenye chakula. Picha na Focus

Na Mwandishi wetu

Wanaume kutoka Kijiji cha Igangidung’u Kata ya Kihanga wilayani Iringa wameeleza namna ambavyo wanafanyiwa ukatili wa kisaikolojia kwa kupewa dawa za kuwapumbaza akili zikifahamika kwa jina la ‘limbwata’ sambamba na kukutana na vipigo kutoka kwa wake zao.

Wakizungumza katika mdahalo wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia ulioandaliwa na Shirika la World Vision kwenye Kata ya Kihanga wilayani Iringa baadhi ya wanaume wamesema kuwa wamekuwa wakiwekewa limbwata kwenye chakula huku wengine wakidai kukutana na kipigo.

Sauti ya Wanaume

Kwa upande wao baadhi ya wanawake wa kijiji hicho wamesema kuwa wanaume wengi wamekuwa wakifanyiwa matukio ya ukatili.

Sauti ya Wanawake

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Iringa  Bi. Gladness Amulike amekiri kuwepo kwa ukatili wa kihisia sambamba na ukatili wa kimwili katika jamii.

Sauti ya Afisa Maendeleo

MWISHO