Nuru FM

Wagonjwa 4200 wahudumiwa katika Kambi ya Madaktari wa Samia Mkoani Iringa

7 December 2024, 11:02 am

Picha ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za kibingwa Mkoani Iringa. Picha na Ayoub Sanga

Na Mwandishi wetu

Historia imeandikwa katika Mkoa wa Iringa baada ya wananchi zaidi ya 4200 kuhudumiwa pamoja na wagonjwa zaidi ya 150 kufanyiwa upasuaji kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Dkt.Samia walioweka kambi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Akifunga kambi hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mh.Ibrahim Ngwada amesema anamshukuru Mh Rais kwa uwekezaji Mkubwa katika Sekta ya afya uliofanywa ambao unarahisisha wananchi kupata matibabu katika kambi hizi.

Sauti ya Ngwada

Naye Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Dkt.Aman Malima amesema uwepo wa kambi hizi unasaidia kubadilisha maisha ya watu wenye changamoto za kiafya na kuwarudishia tabasamu pamoja na kuongeza ushirikiano katika utendaji kazi kwa watumishi.

Sauti ya Malima

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt.Alfred Mwakalebela amesema kambi hizo zinawasaidia wananchi kutosafiri umbali mrefu na kuweza kupata matibabu kwa urahisi.

Sauti ya Mwakalebela

Kwa upande wao baadi ya wananchi waliofika kupata huduma za kitabibu katika hospitali ya Rufaa Iringa wameishukuru serikali kwa kuwapatia huduma hizo huku wakiomba liwe zoezi endelevu.

Sauti ya Wananchi

Kambi ya Madaktari Bingwa wa kanda ya Kati inayojumisha Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Dodoma,Tumbi,Morogoro Singida na Iringa imemalizika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa tarehe 06/12/2024

mwisho