Maambukizi ya VVU Iringa yapungua kutoka 11.3 mpaka 11.1%
4 December 2024, 11:09 am
Na Hafidh Ally
Maambukizi ya Ukimwi Mkoa wa Iringa maambukizi ya virusi vya ukimwi mkoa wa iringa yapungua kutoka 11.3% mpaka 11.1% kwa mwaka 2020- 2023.
Hayo yamezungumzwa na Mratibu wa huduma za kudhibiti Ukimwi Mkoa wa Iringa Prizantus Ngongi na kuongeza kuwa hatua hiyo imetokana na uwepo wa tafiti sahihi za Maambukizi ya VVU.
Amesema kuwa wanatumia tafiti sahihi za maambukizi ya ukimwi ili kutekeleza mpango mkakati wan chi katika kutoa huduma sahihi za kupunguza maambukizi mapya.
Waziri wa Afya Mh. Jenista Mhagama amesema kuwa zaidi ya Bilion 750 zimetumika hapa nchini kwa ajili ya kufubaza maambukizi ya Ukimwi.
Naye Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango ameitaka jamii kuachana na tabia hatarishi ikiwemo ulevi uliopindukia, matumizi ya dawa za kulevya na ngono zembe ili kuepuka maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI ambayo husababisha kupoteza nguvu kazi.
Wastani wa chini wa maambukizi ni katika mikoa ya Zanzibar lakini kwa mkoa ya Tanzania Bara wenye maambukizi ya chini ni Kigoma wenye asilimia 1.7.
MWISHO