Vijana Iringa waaswa kuacha kubeti
3 December 2024, 8:43 am
Na Halima, Aisha, Zahara na Shahanazi
Viongozi wa dini mkoani Iringa wamewaasa vijana kuacha kujihusisha na shughuli zisizo halali kama michezo ya kubashiri na Kamari na badala yake kufanya shughuli zingine halali za kujiingizia kipato .
Hayo yamezungumzwa na Mchungaji wa kanisa la KLPT Mchungaji Stanley Kiyeyeu amesema kuwa michezo ya kubashiri na kamali ina madhara makubwa katika jamii kwani hupelekea vijana wengi kujihusisha na mambo maovu kama vile uvutaji bangi, zinaa na ulevi.
Naye Shekhe Sadick shaweji amewaasa vijana kujikita kwenye shughuli halali za uzalishaji mali kwa sababu michezo ya kubashiri na kamali ni haramu katika uislamu na ameeleza hukmu kupitia Quran tukufu.
Kwa upande msimamizi wa Michezo ya Kibashiri kutoka Taasisi ya Meridian bet Bw. Joseph Nicholous iliyopo mashine tatu mkoani Iringa amesema vijana hawafanyi kazi za uzalishaji mali na kujihusisha katika michezo ya kamari na kubashiri kutokana na ukosefu wa ajira.
Nao vijana wanaojihusisha na shughuli za michezo ya kamari ya kubashiri Mkoani Iringa wamesema wanafanya michezo hiyo kama sehemu ya burudani sambamba na kuvutiwa kutokana na timu zao za mipira, ukosefu wa ajira na baadhi wakidai kuendelea kucheza ili kurudisha fedha walizopoteza wakati wakicheza.
MWISHO